Wednesday, September 3, 2014

New Track: Mackapizzo MC-Pambana kila siku Mp.3

Wednesday, November 20, 2013

A.Y AAMUA KUTIMIZA NDOTO YA KUWA RUBANI,AINGIA SHULE RASMI.

Ni ngumu sana kwa mtu maarufu, mwenye hela na uwezo wa kilakitu anchohitaji kuamua kutimiza ndoto
aliyokuwa nayo kitambo. Lakini hii inaenda kutokea kwa mkali A.Y 'Ambwene Yesaya' ambaye ameamua kurudi Chuo na kufanya kitu ambacho alikuwa anakitamani long time kitambo. Lakini hii haimaanishi kuwa mchizi anaacha muziki. Kwasasa A.Y amesha lipa ada ya hiyo kozi katika  Chuo cha Mafunzo ya Urubani cha ‘Mosswood Aviation Academy’ kilichopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) na anatarajia kuanza masomo Januari 2014.Amefunguka hayo kupitia Mwananchi Hili ni bonge la concept kutoka kwa mchizi na ni mfano bora. All the best bro.

Thursday, October 31, 2013

Mariah Carey na Nas wapiga collabo kali

Mapema Mwaka huu Mdada Mariah Carey aliweka teaser juu ya albam yake ijayo iitwayo 'The Art of Letting Go', lakini alichelewa kuiachia hiyo albam kama alivyoahidi ili kukamilisha mambo kadha wa kadha. Moja kati ya hizo sababu za ukamilishaji ni pamoja na kuijumuisha ngoma anayofanya na Mkali Nas.Naamini itakuwa ni bonge la collabo.Msikilize yeye mwenyewe Mariah Carey akifunguka.

Tuesday, October 29, 2013

EMINEM NA RIHANA KUFANYA NGOMA MPYA YA PAMOJA TENA 'MONSTER''

Kwa mara ya kwanza Rihana 'Riri' na Eminem walitisha sana kwa ngoma ya 'Love the way you lie', Jana October 28, Eminem ameweka wazi kuwa wanaachia ngoma nyingine iitwayo 'Monster' ambayo inatabiriwa makubwa katika soko.
Ngoma inaanza kwa Acoustic guitar na Rihana ananzaa kwa kuimba maneno haya "I'm friends with the monster that's under my bed/ Get along with the voices inside of my head/ You trying to save me, stop holding your breath," Ni ngoma kali in short.

CHRIS BROWN AACHIWA BAADA YA KUSOTA JELA MASAA 36

Hatimae Chris Brown ameachiwa huru baada ya kusota jela kwa zaidi ya masaa 36 kutokana na shambulio alilolifanya kwa mtu nje ya Night Club.
Breezy na Bodyguard wake walikamatwa Juzi Jumapili asubuhi baada ya kumchapa jamaa aliyefahamika mahakamani kwa jina la Parker Adams mwenye umri wa miaka 20. Jamaa amesema mahakamani kuwa alikuwa anataka kupiga picha na Breezy ghafla akastukia akitupiwa sumbwi na breezy.
Kwa mujibu wa Mahakama Chris Brown na Bodyguard wake wamekutwa hawana hatia na wameachiwa huru.ila wameamriwa kurudi mahakamani Novemba 25 na kukaa umbali wa yard 100 na jamaa aliyewashtaki.

Monday, October 28, 2013

Kwanini Jay-Z na NAS ni mfano wa kuigwa kwenye Hip hop???

Wakali ambao wana historia za kipekee kwenye ulimwengu wa Hip hop Nasir Jones Escoba 'Nas' na Sean Carter 'Jay -Z' ni mfano mzuri wa kuigwa katika ulimwengu wa Hip hop. 
2005- Ulikuwa ni mwaka ambao kulikuwa na bifu kali ya Jay-Z na Nas katika ulimwengu wa Hip hop. Baada ya Jay-Z kumponda Nas kwenye tamasha la Summer Jam 2001 na kutoa album aliyoiita 'Take over' to the world, Jay Z na Nas waliingia kwenye vita kali ya mashairi,kama vile Take over ya Jay-Z vs Ether ya Nas, Ether vs Super Ugly, Super ugly vs The Last Real Nigga Alive na Blue print2.  Kilichofurahisha katika bifu ya Jay Z na Nas ni kwamba bifu ilitengeneza Great Music na haikuwa kama bifu zinazo ibuka miaka ya hivi karibuni. Na bifu ya Jay na Nas ndo bifu ambayo kwa upande wangu nadhani inafaa kuwa mfano kwa wasanii wasasa wa Hip hop.
Mnamo October 27, 2005, katika tamasha la Powerhouse Concert  lililoandaliwa na  kituo cha radio 105.1 ndipo ambapo bifu ya Jay-Z na Nas ilikua officialy squashed pale Nas alipo tokea kwenye show ya Jay-Z bila kutarajiwa. Na hapo kwa makusudi jina la show likabadilika na kuitwa 'I declare War' yani 'Natangaza Vita'. Watu wengi mashabiki wa Jay walitegemea Jay angejipanga kwa mashairi ya vita dhidi ya adui yake 'Nas'. Badala yake Jay-Z aligeuka na kupanda stejini akiwa na adui yake Nas na kuperform ngoma ya 'Dead Presidents' na 'The World is Yours'. Baada ya Performance Jay na Nas wakapeana mikono na ukawa ndo mwisho wa Bifu yao. Hapo ndipo unapata picha kuwa ile 'I Declare War' ni kinyume cha 'I Declare Peace'.
Mnamo Januari 2006,  Jay-Z na Nas  wame make headlines baada ya Jay kumsaini Nas kuingia Def Jam wakati Record label ikiwa chini ya Hov. 'Jay-Z'.  Nas aliendelea kushirikiana na Jay  katika  album ya Hip hop is dead  kupitia ngoma ya 'Black Republicans' na kwa mara nyingine mwaka 2007 wametoa ngoma ya 'Success'.
Huu ni mfano mzuri kwa wana hip hop wa sasa kujifunza namna ya bifu za kujenga.

CHRIS BROWN ATIWA NGUVUNI KWA KUMTUPIA MASUMBWI MTU

Mkali Chris Brown 'Breezy' Jana mida ya saa 4 asubuhi amekamatwa na makachero kwa kosa la kumchapa makonde jamaa mmoja ambaye inasemekana hawajuani. Taarifa zilizopatikana kutoka mtandao wa TMZ zinasema Mchizi Breezy aliingia kwenye majibizano na mchizi mwingine nje ya Hotel, huku na huku Breezy si  akamrushia jamaa Konde la uso na inasemekana aliyepigwa hajarudishia mashambulizi. Breezy alikamatwa na kutupwa sero akiwa na Bodyguard wake.
Breezy bado yupo kwenye maangalizi ya kesi ya kumshambulia Rihana na ameongeza ishu nyingine. By the way kinachonishangaza kwa Breezy ni kwamba hivi alimuajira Bodyguard afnye kazi gani iwapo mpango wa ngumi anausimamia mwenyewe. LOL!!!

Saturday, September 14, 2013

Francis Cheka kujengewa nyumba ya Kisasa na Serikali

Baada ya kumtwanga Mmarekani Phil Williams katika Masumbwi na kutwaa ubingwa wa Dunia, Mkali Francis Cheka sasa kujengewa nyumba ya kisasa na serikali kama sehemu ya pongezi kwa ushindi huo.
Ahadi hiyo imetolewa Jana Trh. 13 Sept. 2013 na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera kwa niaba ya serikali wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Mkali huyo Mjini Morogoro. Hongera sana Cheka. U deserve Bro.